PSG yailaza Barcelona kwa mabao 3 kwa 2

Blaise Matuidi akishangiliwa baada ya kupachika bao la tatu dhidi ya Barcelona
Blaise Matuidi akishangiliwa baada ya kupachika bao la tatu dhidi ya Barcelona

Klabu ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa imehcaraza Barcelona kutoka uhispania kwa mabao 3 kwa 2. PSG ilikuwa nyumbani katika hatuwa ya kwanza ya kuwania ubingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Katika mechi hiyo ambayo ilitawaliwa kwa sehemu kubwa na Barcelona, wachezaji wa kocha Laurent Blanc walionyesha ukakamavu. Hadi mapunziko PSG ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2 kwa 1 yalipachikwa nyavuni na Luiz pamoja na Verratti ktika uwanja wa Parc des Princes.

Katika kipindi cha pili mchezaji Matuidi aliwapa furaha mashabiki wa PSG waliokuwa wamefurika kwa wingi kwa kupachika bao la 3, lakini mchezaji kutoka Brazil Neymar akawapa nafasi Barcelona ya kupunguza uzito wa ma bao kwa kupachika bao la pili

PSG kwa sasa inaongoza katika kundi F baada ya ushindi huo, na kujiweka sawa baada ya kuboronga katika ligi kuu nchini Ufaransa.

Baada ya mechi hiyo Mshambuliaji Matuidi amewambia waandishi wa habari kwamba ushindi huo ni muhimu na inaonyesha kiasi gani PSG ni timu kubwa, kwa sasa kinachobaki ni kuonyesha ukubwa huo kwenye ligi kuu.