AFRIKA-SOKA-MICHEZO

CAN 2015: Côte d’Ivoire yaibwagiza DRC mabao 2-1

Wilfried Bony (katikati) wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014.
Wilfried Bony (katikati) wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014. REUTERS/Brian Snyder

Timu ya taifa ya Côte d’Ivoire imeishinda Jumamosi Oktoba 11 mwaka 2014 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mjni Kinshasa, mwezi mmoja tu baada ya kufungwa na Cameroon mabao 4-1.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Cameroon imekwenda sare ya kutofungana na Sierra Leone.
Cameroon inaongoza katika kundi la D ikiwa na alama 7, ikifuatiwa na Côte d’Ivoire, ambayo ina alama 6.

Côte d’Ivoire haikukataa tamaa baada ya kushindwa kufanya vizuri mwezi Septemba ilimenywa na Cameroon mabao 4-1

Katika dakika 17 ya mchezo, Wilfried Bony ameshindwa penalti, baada ya mchezaji wa Congo kufamfanyia madha,bi mchezaji wa Côte d’Ivoire.

Katika dakika 5 za mwisho za kipindi cha kwanza DRC imeshambulia lango la Côte d’Ivoire, bila hata hivo kuingiza mpira wavuni.

Katika dakika 49 mchezaji wa timu ya Côte d’Ivoire aliunawa mpira kwenye eneo la hatari, lakini muamuzi hakupuliza kipenga. Hata hivo katika dakika ya 68, DRC ilisawazisha kwa mkwaju wa penalti uliyowekwa wavuni na beki Cédric Mongongu

Baada ya bao hilo kupitia mkwaju wa penalti, DRC ilikuja juu, lakini Côte d’Ivoire iliendelea kujidhatiti, hadi dakika 83 Alain Gradel akaliona lango la DRC kupitia pasi ya Yaya Touré. Lakini ilmeona wazi kwamba Alain Gradel alikua ameotea.

Kwa sasa Cameroon inaongoza kwa alama 7, ikifuatiwa na Côte d’Ivoire ikiwa na alama 6, DRC ikichukua nafasi ya tatu ikiwa na alama 3, huku Sierra Leone ikiburuza mkia ikiwa na alama 1.