URUSI-Kombe la dunia 2018

FIFA yaridhishwa na maandalizi ya Urusi kwa Kombe la Dunia mwaka 2018

Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA, Joseph Sepp Blatter (kushoto) akiwa pamoja na rais wa Urusi, Vladimir Poutine Jumapili Julai 13 mwaka 2014, Rio de Janeiro.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA, Joseph Sepp Blatter (kushoto) akiwa pamoja na rais wa Urusi, Vladimir Poutine Jumapili Julai 13 mwaka 2014, Rio de Janeiro. REUTERS/Alexey Nikolsky/RIA Novosti/Kremlin

Wakaguzi wa Shirikisho la soka duniani FIFA, wanasema wamefurahishwa na kuridhishwa na maandalizi ya Urusi kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa waangalizi hao Christian Unger amesema ziara yao ya kwanza nchini Urusi imewapa nafasi ya kuona viwanja vitakavyotumiwa katika mashindano hayo makubwa na maandalizi yanaendelea vizuri.

Wakaguzi hao wamesema kuwa, sasa wanaiwaza Urusi baada ya kukamilika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu.

Kati ya miji sita itakayotumiwa kuandaa michuano hiyo, wakaguzi hao tayari wamezuru miji minne kujionea namna maandalizi hayo yanavyoendelea.