AFRIKA-SOKA-MICHEZO

Namibia: michuano ya soka inayowahusisha wanawake inaendelea

Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria.
Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria. AFRIKSPORT

Leo Jumatano joni Oktoba 22 michuano ya soka hatua ya nusu fainali kutafuta bingwa wa Afrika baina ya wanawake inachezwa jijini Windhoek nchini Namibia.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa watetezi, Nigeria muda si mrefu watachuana na Afrika Kusini katika uwanja wa Kimataifa wa Sam Nujoma na baadaye saa tatu usiku saa za Afrika Mashiriki sawa na saa mbili usiku saa za Afrika ya Kati, Cameroon watachuana na Cote d'Ivoire.

Hadi sasa raia wa Nigeria, Desire Oparanozie, ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa mabao, na hadi sasa amefunga mabao manne.

Fainali itachezwa siku ya Jumamosi.

Washindi wa kwanza katika michuano hii wataliwakilisha bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia baina ya wanawake mwaka ujao nchini Canada.