Pata taarifa kuu
ALGERIA-Soka Barani Afrika

Algeria: Setif yanyakua taji la klabu bingwa Afrika

wachezaji wa Es Setif wakati wa mchuano na klabu ya Espérance ya tunisia mwezi Mei mwaka 2014.
wachezaji wa Es Setif wakati wa mchuano na klabu ya Espérance ya tunisia mwezi Mei mwaka 2014. AFP PHOTO / SALAH HABIBI
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Klabu ya Es Setif ya Algeria mwishoni mwa juma liliyopita ilinyakua taji la klabu bingwa barani Afrika baada ya sare ya bao 1 kwa 1 na klabu ya AS Vita club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Entente Setif ya Algeria, imeshinda Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza katika miaka 26 baada ya kuimenya AS Vita Clubkutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 3 kwa 3 Jumamosi Novemba 1.

Mechi ya awali iliyochezwa mjini Kinshasa wiki moja iliyopita timu hizo mbili zililazimika hadi kipenga cha mwisho kutoka sare ya mabao2 kwa 2.

Klabu ya Setif ilifunga bao la kwanza baada ya dakika nne za kipindi cha pili cha mchezo kupitia Sofiane Younes, ambaye alipewa pasi na El Hadi Belameiri baada ya mabeki wa As Vita club kushindwa kumzuia mchezaji huyo nyota wa Setif. Lakini As Via Club ambao walikua wageni nchini Algeria walisawazisha katika dakika ya tano tu baadaye kupitia mchezaji Lema Mabidi, ambaye aliingiza bao hilo akiwa nje kidogo ya eneo la hatari la Setif.

Mabidi aliifungia timu yake mabao mawili wiki moja iliyopita katika mechi ya ufunguzi mjini Kinshasa.

Timu za Algeria zimeendelea vizuri mwaka 2014, baada ya timu ya taifa ya nchi hiyo kushiriki Kombe la dunia 2014 nchini Brazil, ambayo iliondolea katika mzunguko wa pili katika michuano ya Kombe hilo mwezi Juni mwaka 2014.

As Vita club ilifanikiwa kubeba Kombe la michuano hiyo mwaka 1973 na ilionekana pia kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka 1981, wakati ilikuwa bado inajulikana kama mabingwa wa Kombe la Afrika. Entente Setif sasa itashiriki mwezi ujao michuano ya Kombe la Dunia katika nchi jirani ya Morocco.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.