SOKA-MICHUANO YA KLABU BINGWA UEFA

Manchester City yaiburuza AS Roma

Kufuatia bao la Samir Nasri, Manchester City imefaulu kutinga katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuichapa AS Roma mabao 2-0 katika uwanja wa Roma. Jumatano Desemba 10 mwaka.
Kufuatia bao la Samir Nasri, Manchester City imefaulu kutinga katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuichapa AS Roma mabao 2-0 katika uwanja wa Roma. Jumatano Desemba 10 mwaka. FP PHOTO / GABRIEL BOUYS

Katika uwanja wa AS Roma, Manchester City ilijinyakuliwa ushindi katika mzunguko wa nane wa fainali ya Ligi ya Mabingwa kufuatia bao la ajabu lilowekwa wavuni na Samir Nasri. Hadi kipenga Manchester imekuaikiongza kwa mabao 2-0 dhidi ya AS Roma.

Matangazo ya kibiashara

PSG imeshindwa kufanya vizuri ikiwa ugenini na kukubali kupigwa na Barcelona mabao(3-1).

Ushindi dhidi ya AS Roma ulikuwa ni muhimu kwa Manchester City ili itinge mzunguko wa nane wa fanali ya Ligi ya Mabingwa.

Mabingwa wa Uingereza hawakutetereka wakiwa ugenini katika uwanja wa As Roma. Wachezaji nyota wa Manchester City kama Samir Nasri ambaye aliingiza bao la kwanza pamoja na Zabaleta, ambaye alikamiliza ushindi wa Manchester City kwa kuweka wavuni bao la pili katika dakika 87.

Katika Kundi F, PSG imelazimika kupigwa mabao 3-1 ikiwa ugenini katika uwanja wa Barcelona. Lionel Messi, Zlatan Ibrahimovic, Neymar na Suarez hawakuambua kitu, hata kama Messi alijitahidi kufanya vizuri, na kusawazisha katika dakika ya nne baadaye. Messi kwa sasa amevunja rekodi kwa kutimiza mabao 76 aliyoingiza kwa guu lake. Hata hivyo Barcelona walikuja juu hadi dakika ya mwisho ya mchezo. PSG walisalimu amri na kujikuta wamebwagizwa mabao 3-1.

Kungineko Chelsea imeiburuza Sporting Lisbon kwa mabao 3-1. Katika kundi H, Porto na Donetsk walitoka sare ya kufungana bao 1-1. CSKA Moscow walilala kwa kuchapwa goli 3-0 na bayern munich, Ajax walipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Apoel Nicosia, Schalke 04 imemchapa 1-0 Maribor huku Athletic Bilbao wakiwabanjua BATE Borisov kwa goli 2-0.

Klabu ambazo zimetinga katika hatua ya mtoano ni 16. Klabu zinazochukua nafasi ya kwanza katika makundi na ambazo bado zina mchezo wa marudio ni 8:

Real Madrid
AS Monaco
Borussia Dortmund
Bayern Munich
FC Barcelone
Chelsea
Porto

Klabu ambazo zimejikuta zikiangukia kwenye ligi ya Europa baada ya kushindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano ni 8:

Olympiakos
Liverpool
Zénith St-Pétersbourg
Anderlecht
AS Rome
Ajax Amsterdam
Sporting Lisbonne
Athletic Bilbao

Droo ya upangwaji ratiba kwa michezo ya kumi na sita bora itapangwa Jumatatu Desemba 15 hatua ya mtoano itaendelea tena Februari.