SOKA-UFARANSA-ARSENAL-HENRY

Baada ya kujizolea sifa, Thierry Henry astaafu

Mwaka 2012, Thierry Henry alirejea Arsenal kwa mkopo na kufunga mara mbili.
Mwaka 2012, Thierry Henry alirejea Arsenal kwa mkopo na kufunga mara mbili. AFP PHOTO/IAN KINGTON

Taarifa hii imekua ikisubiriwa tangu majuma kadhaa yaliyopita. Kwa sasa taarifa hiyo imekua rasmi: Thierry Henry amechukua uamzi wa kustaafu katika ulimwengu wa soka.

Matangazo ya kibiashara

Thierry Henry, mwenye umri wa miaka 37, nyota wa Arsenal, mfungaji bora wa timu ya ya taifa ya Ufaransa, ameamua kustaafu baada ya kushiriki soka kwa kipindi cha miaka 20. Thierry Henry ameyasema hayo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Thierry Henry alianza kupata sifa akichezea klabu ya Arsenal katika miaka ya 2000. Mchezaji huyu aliingiza mabao 228 katika mechi 377 tangu alipoanza kucheza hadi siku ya leo alipo tangaza kustaafu.

Mbali na kuchaguliwa kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry alichezea Arsenal kwa kipindi kirefu, aliiva nambari 14 mgongoni kwa kipindi cha miaka minane, baada ya miaka mingi akipata mafunzo katika klabu ya Monaco, ambapo mechi yake ya kwanza katika klabu ya Monaco aliicheza mwaka 1994.

Thierry Henry ni mfungaji bora anaye ongoza nafasi ya pili katika kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA), na mchezaji bora nchini Ufaransa mwaka 1997. Thierry Henry aliichezea pia klabu ya Juventus kwa kipindi cha miezi saba na kupelekea ushindi wa klabu hiyo wa Kombe la Intertoto.

Thierry Henry ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani, na mrithi tosha wa Dennis Bergkamp, ambaye bado ni mchezaji wa kihistoria nchini Uingereza. Mei 7 mwaka 2006, Thierry Henry aliifungia kwa guu lake klabu ya Arsenal, ikichezea nyumbani, mabao 3 dhidi ya Wigan, ambayo wakati huo ililazimika kukubali kuchapwa mabao 4-2.

Raia huyo wa Ufaransa, amemstaafu akiichezea klabu ya New York Red Bulls ya Marekani na sasa atakuwa mchambuzi wa soka katika runinga ya Sky Sports.

Historia fupi ya Henry :

1994 Alijiunga na klabu ya Monaco akiwa na umri wa miaka 17

1998 Hakucheza wakati Ufaransa iliponyakua kombe la dunia

1999 Alijiunga na klabu ya Juventus na kuichezea mara 20

1999 Alijiunga na Arsenal na kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji mawili ya klabu bingwa nchini Uingereza na mataji matatu ya kombe la FA.

2000 Aliifungia Ufaransa mabao matatu na kuisaidia kunyakua taji la Euro.

2007 Alijiunga na Barcelona kwa kima cha Paundi Milioni 16.1

2009 Aliisaidia Barcelona kushinda ligi na klabu bingwa barani Ulaya

2010 Alijiunga na New York Red Bulls

2012 Alirejea Arsenal kwa mkopo na kufunga mara mbili