LA LIGA-UHISPANIA-FC BARCELONA-CAS-FIFA

CAS yapigilia msumari wa mwisho kwa klabu ya FC Barcelona kutofanya usajili hadi 2016

Wachezaji wa FC Barcelona
Wachezaji wa FC Barcelona REUTERS/Juan Medina

Klabu ya FC Barcelona ya nchini Uhispania haitaruhusiwa kufanya usajili wa mchezaji yeyote kwa mwaka 2015 baada ya rufaa yao kupinga uamuzi wa awali wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kutupwa na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo CAS. 

Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Barcelona ilifungiwa kwa muda wa miezi 14 mwezi A[ril mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria za Fifa kuhusu masuala ya usajili wa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 18.Fifa rejected an appeal in August but the pending appeal to Cas allowed Barca to sign players including Luis Suarez.

Kwa mujibu wa shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa, limedai kuwa klabu hiyo ilienda kinyume na sheria kwa kusajili wachezaji walio chini ya umri wa miaka 18 na kuwatumia kwenye mashindano kati ya mwaka 2009 na 2013.

Kwenye hukumu yake, CAS imesema kuwa, jopo la majaji waliosikiliza rufaa hiyo wamekubaliana pasipo na mashaka kuwa, Barcelona ilienda kinyume na kanuni za Fifa kwa kutumia wachezaji hao kinda kwenye mashindano na kwenye akademi yake ya vijana na hivyo hukumu ya Fifa itasalia kuwa pale pale.

Mara baada ya hukumu hiyo klabu ya Barcelona kupitia kwenye tovuti yake imeandika "Makosa ambayo klabu inaweza kuwa imeyafanya na ambayo yanatambulika na kuwasilishwa kwenye vyombo husika yako kotekote, kiutawala na kwakiasi kikubwa yamechangiwa na muingiliano wa sheria za Fifa na zile za Uhispania na kwakuzingatia kuwa klabu yetu ilikuwa sahihi". Imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa "Kwahivyo basi FC Barcelona inaona hukumu hii haikuwa ya haki na imelenga kuikomoa timu yetu wakati unapolitazama suala hili na mazingira yenyewe yaliyojitokeza". Ilimaliza taarifa hiyo.

Wakati klabu ya Barcelona ikisubiri uamuzi wa rufaa yake CAS, wakati wa dirisha la usajili wa majira ya joto ilitumia kiasi cha euro milioni 150 sawa na pauni za Uingereza milioni 117 kufanya usajili wa wachezaji Luisi Suarez, Ivan Rakitic, Marc-Andre ter Stegen, Thomas Varmaelen, Claudio Bravo, Jeremy Mathieu na Alen Halilovic.