SOKA-LIGI KUU YA UINGEREZA

Swansea yaburuzwa na Liverpool

Meneja wa liverpool, Brendan Rodgers (kulia) akimpongeza mchezaji wake Adam Lallana.
Meneja wa liverpool, Brendan Rodgers (kulia) akimpongeza mchezaji wake Adam Lallana. REUTERS/Phil Noble

Nchini Uingereza, klabu ya soka ya Liverpool imepata ushindi mkubwa wa mabao 4 kwa 1 dhidi ya Swansea katika mechi ya ligi kuu ya soka nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Liverpool walipata ushindi huo mkubwa wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Anfiield.

Bao la kwanza la Liverpool lilifungwa na Alberto Moreno katika dakika ya 33 kipindi cha kwanza, na baadaye Asam Lallana kuwapa Liverpool bao la pili katika dakika ya 51, na kufunga la tatu dakika kumi baadaye.

Dakika nane baadaye, mkwaju wa Asam Lallana katika dakika ya 69 ulimtatiza mchezaji wa Swansea Jonjo Shelvey aliyejifunga mwenyewe kwa kuelekeza kichwa katika goli lao.

Bao pekee la Swansea lilifungwa na Gylfi Sigurdsson .

Liverpool wanamaliza mwaka kwa ushindi mkubwa, lakini Swansea wamefungwa kwa mara ya kwanza ndani ya michezo mitatau iliyopita.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgerss, amefurahia ushindi huo na kusema licha ya vijana wake kuoneakana kuwaachia mipira wapinzani hasa katika kipindi cha kwanza, walicheza vizuri na kupata ushindi mkubwa.

Liverpool kwa sasa ni ya nane kwa alama 28, huku Chelsea ikiongoza kwa alama 46.