COTE D'IVOIRE-SOKA-MICHEZO-CAN 2015

Mashabiki wa Cote d'Ivoire walalamikia viza

Mashabiki wa Cote d'Ivoire wakipigwa picha wakati wa mechi ya kufuzu dhidi ya Sierra Leone, Novemba 14 mwaka 2014 katika mji wa Abidjan.
Mashabiki wa Cote d'Ivoire wakipigwa picha wakati wa mechi ya kufuzu dhidi ya Sierra Leone, Novemba 14 mwaka 2014 katika mji wa Abidjan. AFP PHOTO / SIA KAMBOU

Michuano ya 30 ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) yanatazamiwa kuanza tarehe 17 Januari mwaka 2015.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Côte d’Ivoire, mashabiki wa timu ya taifa ya Côte d’Ivoire wamekua wakipata mafunzo ya jinsi watakavyoshabikia timu hiyo ya taifa wakati wa michuano hiyo itakayochezwa Equatorial Guinea.

Hata hivyo mpaka sasa bado hawajawa na uhakika wa kupata viza zao, wakati ambapo utaratibu bado ni ngumu. RFI ilitembelea moja ya eneo la mazoezi mashabiki hao mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa zaidi ya miezi miwili, mashabiki hao wa timu ya taifa ya soka ya Côte d’Ivoire wamekua wakikutana kila wiki katika mazoezi ya kuimba na mambo mengine, ambayo yatapelekea timu yao inakua na motisha katika michuano hiyo.

Kamati ya Taifa inayohusika na kuunga mkono timu ya taifa ya soka ya Côte d’Ivoire (CNSE) ipo tangu mwaka 1981. Taasisi halisi, ambayo Pulchérie Somplei ni mwanachama kwa karibu miaka 30.

" Inabidi kuwepo na hatua mpya ili tuandamane na timu yetu kwa kuiunga mkono hadi mwisho", amesema Somplei.

" Hii ni muhimu sana. Tangu mwaka 1985, nililishiriki katika michuano kadhaa ya CAN, Kombe la Dunia, na michuano mingine, tunarejelea kila wakati, kwa sababu tunaipenda, tutawashabikia Temboili wapate ushindi", ameendelea Somplei.