Sako akabiliwa na vikwazo vya FIFA
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka duniani FIFA inachunguza ni kwanini mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal na klabu ya West Ham nchini Uingereza Diafra Sakho, alikataa kuichezea timu yake ya taifa ya Senegal katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika.
Diafra Sakho aliamua kujiondioa katika kikosi cha timu ya taifa kilichokuwa kinashiriki katika michuano inayoendelea ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Equatorial Guinea.
Sakho mwenye umri wa miaka 25 alisema alijiodoa katika kikosi cha Senegal kwa sababu ya jeraha la mgongo lakini alioneakana akichezea klabu ya West Ham na kuifungia wakati wa mchuano wa kuwania taji la FA dhidi ya Bristol City, mchuano ambao West Ham ilipata ushindi wa bao moja kwa bila, bao lililofungwa na mchezaji huyo.
Sheria za FIFA zinaeleza kuwa mchezaji hawezi kuichezea klabu yake, wakati akihitajika kuichezea timu yake ya taifa.