MICHUANO YA LIGI YA UINGEREZA-ANFIELD

Liverpool yaiburuzaTottenham kwa 3-2

Wachezaji wa Liverpool wakifurahia ushindi wao.
Wachezaji wa Liverpool wakifurahia ushindi wao.

Klabu ya Liverpool imepata ushindi katika mchuano wake uliyochezwa Jumanne jioni dhidi ya Tottenham kwa kuimenya mabao 3-2, katika michuano ya Anfield ya kuwania nafasi nne za juu za msimamo wa ligi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Goli la kwanza la Mario Balotelli katika michuano ya ligi kuu ya Uingreza limeipa Liverpool ushindi muhimu dhidi ya Tottenham kuwania nafasi ya nne, ambayo ni nafasi muhimu katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Lazar Markovic aliipatishia Liverpool bao la kwanza, ambalo lilirudishwa na Harry Kane wa Tottenham.
Baada ya mapumziko, Steven Gerrard aliipatishia Liverpool bao la pili. Hata hivyo, Tottenham ilikuja juu, kufanikiwa kusawazisha.

Bao hilo la kusawazisha liliwekwa kimyani na Mousa Dembele, kabla ya Mario Balotelli wa Liverpool kuzifuma nyavu na kuifanya klabu yake kupata ushindi wa mabao matatu kwa mawili.
Katika mechi nyingine, Arsenal imepanda ngazi kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Leiceter City mabao 2-1.

Mabao hayo mawili ya Arsenal yaliingizwa na Laurent Koscielny na Theo Walcott, baada ya kupewa mipira mizuri na Mesut Ozil. Arsenal imeshika nafasi ya nne, iliyokua ikishikiliwa na Mancheater United.