LIGI YA MABINGWA / ULAYA

Ligi ya Mabingwa: Wenger akutana na Monaco

Klabu ya Arsène Wenger, Arsenal inajiandaa kukutana Jumatano Februari 25 na klabu ya Ufaransa ya Monaco katika mzunguko wa nane wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, mchuano ambao utakua tofauti na michuano mingine iliyopigwa hivi karibuni.

Arsène Wenger, meneja wa Arsenal.
Arsène Wenger, meneja wa Arsenal. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Arsène Wenger ni meneja wa Arsenal kwa kipindi cha miaka 18 sasa. Klabu ya Monaco itakua ikicheza mchuano huo ikiwa ugenini.

Arsène Wenger, mwenye umri wa miaka 65, aliinoa klabu ya Monaco kwa kipindi cha miaka 7 (tangu mwaka 1987 hadi mwaka 1994).

Arsène Wenger alianza kuino klabu ya Arsenal tangu mwaka 1996. Arsène Wenger aliifikisha klabu ya Monaco kwa mara ya kwanza katika fainali mwaka 1992.

Pamoja na Alex Ferguson, meneja wa Manchester United, Arsène Wenger ni kocha ambaye ana muda mrefu katika Ligi Kuu. Na ni kocha kutoka Ufaransa, ambaye analipwa kitita kikubwa cha pesa.

Kwa mujibu wa France Football, Arsène Wenger anapata Yuro milioni 10 kwa mwaka.