PSG-BAYERN MUNICH-UEFA-SOKA

PSG na Bayern Munich zaingia robo fainali

Mbrazilia David Luiz.
Mbrazilia David Luiz. Reuters / Stefan Wermuth Livepic

Paris Saint Germain imetinga katika robo fainali ya michuano ya Kombe la UEFA, Jumatano Machi 11 mwaka 2015 mjini London.

Matangazo ya kibiashara

PSG imtoka na Chelsea kwa kufungana mabao 2-2. Lakini msindi ilibidi apatikane katika dakika thelathini za nyongeza baada ya dakika tisini za kawaida kumalizika huku timu zote zikiwa zimefungana goli moja kwa moja.

PSG ilicheza dakika 90 ikiwa na wachezaji kumi uwanjani dhidi ya wachezaji kumi na mmoja wa Chelsea, baada ya kuondolea uwanjani mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.

Hadi dakika 90 za kwanza zinamalizika Chelsea 1 na Paris St. Germain 1 na hivyo kulazimika kucheza dakika 30 nyingine ili kumpata mshindi.

Paris Saint Germain imepata ushindi huo kutokana na magoli ya ugenini iliyoyafungajJumatano jioni wiki hii, ambayo magoli mawili kwa miwili lakini magoli ya ugenini iliyoyafunga hapo jana ndio yaliinufaisha, na kutinga katika robo fainali.

Katika msimu uliyopita Paris Saint Germain iliondolewa katika mashindano na Shelsea.

Hayo yakijiri Bayern Munich imeingia pia katika robo fainali baada ya kuinyeshea mvua ya magoli klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine ambayo imeondoka uwanjani na mzigo wa magoli 7 kwa nunge.