TANZANIA-MISRI-SOKA

Tanzania yamenyana na Misri

Uwanja soka wa taifa wa Dar Es Salaam, Tanzania.
Uwanja soka wa taifa wa Dar Es Salaam, Tanzania.

Timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kucheza na timu ya taifa ya Misri siku ya ijumaa wiki hii majira ya saa 10 kamili jioni, mchezo utakofanyika katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini Dar es salaam.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kimekua katika mazoezi kujiandaa na mchezo huo, ambapo kwa takribani wiki mbili kipo kambini Bamba Beach wakijifua kwa mchezo huo.

Tanzania ilifuzu hatua ya pili baada ya kuiondoa timu ya taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12 -9, na endapo itafanikiwa kuwaota Misri, itafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za soka la Ufukweni zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli mwezi April mwaka huu.

Waamuzi wa mchezo huo ni Eid Haitham Eid Hassan (Sudan), mwamuzi msaidzi wa kwanza Abaker Mohamed Bilal (Sudan), mwamuzi msaidizi wa pili Abdalla Hassain Hassaballa, mtunza muda (time-keeper) Boubaker Bessem (Tunisia) wakati kamishna wa mchezo huo ni Khiba Herbert Mohoanyane kutoka Lesotho.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika wiki ijayo nchini Misri kati ya Machi 20,21 na 22 mwaka huu.