KENYA-SOKA-SHERIA

Kenya: Mahakama yairuhusu KPL kuendelea na ligi

Mahakama jijini Nairobi nchini Kenya imeamua kuwa kampuni ya KPL inaweza kuendelea na ligi yake nchini humo, na kutupilia mbali kesi ya Shirikisho la soka nchini humo FKF.

Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ambako Mahakama imeiruhusu KPL kuendelea na ligi.
Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ambako Mahakama imeiruhusu KPL kuendelea na ligi. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Ni uamuzi ambao umeridhisha viongozi wa KPL na mkurugenzi mkuu wa ligi hiyo, Jack Oguda, amesema ligi yao itaanza haraka iwezekanavyo na kuna michuano ambayo itachezwa katikati ya wiki.

Lakini hii inaamanisha kuwa kutakuwa na ligi mbili nchini Kenya, moja ya KPL na nyingine ya Shirikisho la soka FKF msimu huu.

Huu ni uamuzi ambao unaonekana haukutatua mvutano kati ya KPL na FKF kuhusu ni nani aliye na wajibu wa kusimamia ligi ya soka nchini humo.