JUVENTUS-BARCELONA-UEFA-SOKA

Barcelona na Juventus zafuzu katika robo fainali ya michuano ya UEFA

Barcelonaimeimenya Manchester City kwa bao 1-0 Jumatano jioni Machi 18 mwaka 2015.
Barcelonaimeimenya Manchester City kwa bao 1-0 Jumatano jioni Machi 18 mwaka 2015. REUTERS/Juan Medina

Klabu ya Barcelona ya Uhispani na Juventus ya Italia ni vilabu vya mwisho kufuzu katika robo fainali ya michuano ya kuwani ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya UEFA.

Matangazo ya kibiashara

Barcelona walifunga Manchester City ya Uingereza kwa bao 1 kwa 0 katika mchuano wa marudiano na kufuzu kwa jumla ya mabao 3 kwa 1.

Juventus nao walifuzu kwa kuwasinda Borrus Dortumd ya Ujerumani kwa jumla ya mabao 5 kwa 1 na Jumatano wiki hii walipata ushindi wa mabao 3 kwa 0 katika mchuano wa marudiano.

Vilabu ambavyo vimefuzu ni Barcelona, Juventus, Parius Saint Germain, Atletico Madrid, Real Madrid, Bayern Munich, Monaco na Porto.

Droo ya robo fainali itafanyika tarehe 20 mwezi huu.

Kwa upande wa mchezo wa Cricket, Afrika Kusini imefuzu katika hatua ya nusu fainali ya michunao ya kombe la dunia baada ya kuwahdinda Sri Lanka kwa wiketi 9 hapo jana jijini Sydey

Hayo yakijiri rais wa Shirikihso la soka duniani FIFA Sepp Blatter amekataa kushiriki katika mjadala wa runinga kujadili yale anayotaka kuyafanya ikiwa atachaguliwa tena kuwa rais wa FUFA wakati wa uchaguzi utakaofanyika tarehe 29 mwezi wa tano mjini Zurich.

Hata hivyo wapinzani wake watatu Mwanamfalme Prince Ali Bin Al Hussein, Michael van Praag na Luis Figo wamesema wako tayari kushiriki katika mjadala huo.