Droo yatazamiwa kufanyika katika michuano ya soka ya Ulaya
Imechapishwa:
Ijumaa wiki hii kutafanyika droo ya hatua ya robo fainali ya kuwania ubingwa wa klabu bora barani Ulaya UEFA na ligi ya EUROPA.
Katika michuanoa ya UEFA, Vlabu hivyo vinane vilivyofuzu katika hatua hiyo msimu huu ni pamoja na Paris Saint Germain na Monaco za Ufaransa, Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid zote za Uhispania, Porto ya ureno, Beyern munich ya Ujerumani na Juventus ya Italia.
Michuano ya robo fainali itazchwa nyumbani na ugenini, mechi za kwanza zikiwa zitachezwa tarehe 14 na 15 mwezi ujao wa Aprili.
Kwa upande wa ligi ya EUROPA, vlabu amabvyo vimefuzu katika hatua ya robo fainali ni pamoja na Dyna, Kyv, Sevila, Napoli, Club Brugge, Fiorentina, Wolfsburg, Zenit Sain Petersburg na Dnipro Dnipropetrovsk.
Katika mchezo wa Cricket Australia wanamenya na Pakistan Ijumaa wiki hii katika mchuano wa robo fainali kombe la dunia.
Jumamosi Machi 21, New Zeland watapamabana na West Indieis.
India tayari wamefuzu katika hatua ya nusu fainali baada ya kuiwashinda Bangladesh kwa mikimbio 109.
Afrika Kusini pia imefuzu.
Hayo yakijiri Kamati Kuu ya Shirikisho la soka duniani FIFA, imekubali kuahirishwa kwa michuano ya kombe la dunia itakayochezwa nchini Qatar mwaka 2022 kutoka mwezi wa Juni na Julai hadi mwezi wa Novemba na Desemba.
Kamati hiyo imekubali kuwa fainali ya michuani hiyo itachezwa tarehe 18 mwezi Desemba na pia ilikubaliwa kuwa, siku za michuano hiyo itafupishwa kutoka zile za kawaida 28.