UFARANSA-DANEMARK-SOKA ULAYA

Alexandre Lacazette awafungisha kinywa mashabiki wa Denmark

Michuano ya kutafuta tiketi ya kufuzu mashindano ya soka ya mataifa ya Ulaya yanayotaraji kufanyika mwakani iliendelea Jumapili mwishoni mwa juma hili, huku michezo kadha ikipigwa.

Alexandre Lacazette alifunga bao lake la kwanza kwa timu ya Ufaransa Jumapili Machi 29 mwaka 2015 dhidi ya Denmark katika uwanja wa St. Etienne.
Alexandre Lacazette alifunga bao lake la kwanza kwa timu ya Ufaransa Jumapili Machi 29 mwaka 2015 dhidi ya Denmark katika uwanja wa St. Etienne. REUTERS/Robert Pratta
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Ufaransa imeiburuza timu ya Denmark kwa mabao 2-0.

Bao la kwanza la Ufaransa limewekwa wavuni na mfungaji bora katika Ligi kuu ya Ufaransa, Alexandre Lacazette.

Wakati huohuo Ureno walikuwa wenyeji dhidi ya Serbia. Hadi kipenga cha mwisho Serbia ilikubali kichapo cha mabao 2-1. Wakati hayo yakijiri, Hungary imeshindwa kufanya vizuri ikiwa nyumbani baada ya kukubali kutoka sare ya kutofungana na Ugiriki.

Mabingwa wa dunia Ujerumani imeimenya Georgia kwa mabao 2-0, huku Ireland ya kaskazini iikiiadhibu Finland kwa jumla ya mabao 2-1. Scotland iliipa kichapo Gibraltar kwa ushindi wa mabao 6-1, huku Jamhuri ya Ireland ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya Poland.