ALGERIA-GABON-GHANA-CAF-SOKA

CAF yatazamiwa kuchagua mwenyeji wa michuno ya Afcon 2017

Tuzo inayopewa mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Tuzo inayopewa mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Shirikisho la soka barani Afrika linatazamiwa kuchagua Jumatano wiki hii katika mji mkuu wa Misri, Cairo, nchi ambayo itakua mwenyeji wa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Matangazo ya kibiashara

Nchi tatu ikiwa ni pamoja na Algeria, Gabon na Ghana zinagombea nafasi hiyo kwa kuweza kupokea michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika mwaka 2017. Michuano hio ingelichezwa nchini Libya.

Jumatano wiki hii, itajulikana nchi ambayo itakua mwenyeji wa michuano ya awamu ya 31 ya Kombe la mataifa barani Afrika. Shirikisho la soka barani Afrika CAF ambalo litakutana katika mkutano mkuu, litatangaza Jumatano mchana mwenyeji wa michuano hio. Moja kati ya nchi tatu, Algeria, Gabon Ghana itachukua nafasi ya Libya ambayo ilikua ilipangwa kupokea michuano hio. Libya imeondolewa kwenye nafasi hio kutokana na mdororo wa usalama ambao umeendelea kushuhudiwa nchini humo.

Mpaka sasa inafahamika kwamba Cameroon itakua mwenyeji wa Afcon 2019, Côte d’Ivoire 2021 na Guinea 2023.

Misri ilijiondoa mwezi Februari mwaka 2015 kwenye orodha ya mataifa hayo matatu yanayogombea kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika mwaka 2017, kutokana na machafuko yaliyosababisha maafa makubwa katika viwanja vyake vya mpira wa miguu. Hata hivyo Misri ilishatangaza kwamba itaunga mkono Algeria kuwa mwenyeji wa michuano hio.