UEFA-MICHEZO-SOKA

Michuano ya robo fainali ya UEFA yaanza

Timu mbili za Uhispania Atletico Madrid na Real Madrid zinatazamiwa kufungua dimba ya michuano ya robo fainali ya UEFA.
Timu mbili za Uhispania Atletico Madrid na Real Madrid zinatazamiwa kufungua dimba ya michuano ya robo fainali ya UEFA. REUTERS/Michaela Rehle

Michuano ya robo fainali kuwani taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA inaanza kuchezwa leo Jumanne.

Matangazo ya kibiashara

Atletico Madrid ya Uhispania inacheza na Real Madrid pia ya Uhispania, huku Juventus ya Italia ikipambana na Monaco ya Ufaransa.

Michuani hii inachezwa nyumbani na ugenini na baada ya michuano ya juma hili, vlabu hivi vitarudiana tarehe 21 na 22 mwezi huu.

Mara ya mwisho kwa vlabu hivi viwili kukutana katika michuano hii ilikuwa ni wakati wa fainali ya michuano hii mwaka jana, mchuano ambao Real Madrid waliibuka washindi na kunyakua ubingwa na leo itakuwa ni kama marudinao ya mwaka jana.

Leo Jumanne mchuano unaosubiriwa kwa hamu kubwa ni kati ya majirani Real Madrid na Atletico Madrid, vlabu vinavyotoka katika mji mmoja wa Madrid nchini Uhispania.

Kesho Jumatano, Paris Saint Germain watakuwa nyumbani jijini Paris kuwakaribisha Bracelona ya Uhispania, huku Bayern Munich ya Ujerumani wakipambana na Porto ya Ureno.