SOKA-UINGEREZA-MANCHESTER CITY

Matatizo ya Mancher City Uingereza

Kiungo wa kati wa Manchester City, Yaya Touré ( kulia ).
Kiungo wa kati wa Manchester City, Yaya Touré ( kulia ). REUTERS/Eddie Keogh

Ni wazi kuwa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Manchester City wameshakata tamaa ya kutetea ubingwa wao.

Matangazo ya kibiashara

Kinachosalia sasa ni wao kupambana kumaliza katika nafasi nne bora msimu huu ili kufuzu katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya UEFA msimu ujao. Hadi sasa City ipo katika nafasi ya nne kwa alama 64.

Mashabiki wa Manchester City wamekuwa wakijiuliza ni kwanini kiwango cha klabu hii kimeporomoka au kinaendelea kushuka katika siku za hivi karibu ?

Je, ni wachezaji au ni kocha ?

Hii ni klabu ambayo ina wachezaji wa kipekee waliosajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha na wenye hadhi ya juu ukimzungumzia Yaya Toure, Sergio Aguero na, David Silva na wengine wengi.

Wengine pia wanahoji kuwa huenda mbinu za kocha Manuel Pelegrini, zimepitwa na wakati. Lakini pia wale wanaosema kuwa wachezaji wa Mancheter City wamekuwa wazito mno.

Zikiwa zimesalia mechi sita kumaliza msimu wa ligi nchini Uingereza, lawama kati ya wachezaji na wakati mwingine kocha kuwalaumu wachezaji imekuwa ni sababu ya vijana kutoka Etihad kutofanya vizuri msimu huu.

Yaya Touré kiungo wa kati wa Manchester City
Yaya Touré kiungo wa kati wa Manchester City AFP PHOTO / ANDREW YATES

Baada ya kufungwa na Arsenal, Burnely na Manchster United, kocha Pallegrini alimlaumu Yaya Toure kwa kutofanya vizuri katika michuano hiyo na kuongeza kuwa kiwango chake kilikuwa kimeshuka.

Katika hali ya kawaida na ya kibinadamu, mchezaji anapopata lawama kama hizi anaweza kukata tamaa au kupiga moyo konde na kuamua kubadilika lakini inaoneakana Yaya Toure amekata tamaa.

Lakini kinachotokea katika klabu hii ni kitu cha kawaida. Haiwezakani kila wakati unashinda la, mpinzano wako naye mara nyingi atakuwa anajiandaa ili kukufunga na hili tumeliona na Manchster City.

Suala la kumwachisha kazi, kocha Palegrini kwa sbabau ya matokeo mabaya sio suluhu. Kuna wale wanaosema kuwa baada ya kocha wa Borrusia Dortmund ya Ujerumani Jürgen Klopp  kujiuzulu, huenda akapewa kibarua hicho.

Suluhu ya changamoto hii kwa Manchster City ni kwa kocha Palegrini kuwathamini upya wachezaji wake baada ya msimu kumalizika na kufanya maamuzi magumu ya kuwauza baadhi ya wachezaji wake.

Mchezaji kama Yaya Toure amekuwa na mchango mkubwa sana katika klabu hii na msimu uliopita, aliisaidia kunyakua ubingwa lakini inavyoonekana amechoka na huu ndio wakati wa yeye kwenda kuchezaji nje ya Uingereza.

Kumekuwa na mazungumzo ya hapa na pale kuwa huenda Yaya Toure akahamia Inter Milan msimu ujao, na ikiwa ningekuwa katika nafasi ya kumshauri kocha Palegrini, huu ndio wakati wa kuwasajili vijana.

Suluhu sio kumfuta kazi kocha bali ni kumpa nafasi ya kubadilisha kikosi chake na huenda ubingwa ukarejea msimu ujao.