SOKA-UEFA-BARCELONA-BAYERN MUNICH

Barcelona yatinga fainali

Washambuliaji walioiokoa Barcelona Jumanne Mei 12 dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani, Neymar, Luis Suarez na Lionel Messi (kushoto kwenda kulia).
Washambuliaji walioiokoa Barcelona Jumanne Mei 12 dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani, Neymar, Luis Suarez na Lionel Messi (kushoto kwenda kulia). Reuters / Ina Fassbender

Barcelona imetinga fainali ya michuno ya ligi ya Mabingwa, baada ya kumenyana Jumanne usiku wiki hii na Bayern Munich. Bayern Munich imeaga michuano hiyo, baada ya kuifunga Barcelona mabao 3-2 katika mchezo wa marudiano wa michuano ya nusu fainali ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo wa awali uliyochezwa wiki moja iliyopita, Barcelona iliifunga Bayern Munich mabao 3-0.
Barcelona inasubiri kucheza fainali Juni 6 mwaka 2015 na moja ya klabu itakayoshinda leo Jumatano usiku kati ya Real Madrid na Juventus.

Bayern Munich ndio iliyoanza kuona lango la Barcelona katika mchezo wa marudiano wa michuano ya fainali ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya. Bao la kwanza la Bayern limefungwa na mchezaji kutoka Morocco Mehdi Benatia katika dakika ya 7 ya mchezo.

 

Katika dakiaka ya 15 Barcelona kupitia mchezaji wake Neymar ikasawazisha baada ya pasi aliyopewa na Luis Suarez kutoka kwa Muargentina Lionel Messi.

Barcelona iliendelea kushambulia lango la Bayern Munich na kufaulu katika dakika ya 29 kufunga bao la pili kupitia mchezaji wake Neymar, na kuongoza mabao 2-1 dhidi ya Bayern Munich.

Hadi wakati huo, Bayern Munich ilikua inataraji ifunge mabao 6-2 ili iweze kutinga fainali ya michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Lakini hali hiyo haikutokea.

Hata hivyo Bayern ilikuja juu na kufaulu kusawazishabao la pili kupitia Robert Lewandowski katika dakiaka ya 40. .

Katika dakika ya 74, Bayern Munich kupitia mchezaji wake Thomas Müller ilifunga bao la tatu. Hadi kipenga cha mwisho Bayern Munich iliongoza kwa mabao 3-2 dhidi ya Barcelona. Licha ya Bayern kuibuka mshidi katika mchuano huo, ililazimika kuaga michuano hiyo, baada ya kupoteza katika mechi ya awali ya nusu fainali wiki moja iliyopita, ambapo ilifungwa mabao 3-0.

Barcelona, wamefanikiwa kutinga fainali baada ya kuibwaga Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-3 yaliyopatikana katika mikondo yote miwili waliyokutana kwenye hatua ya nusu fainali.

Jumatatu usiku wiki hii kutakuwa na mchuano kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus kwenye uwanja wa Benabeu.