BARCELONA-BILBAO-SUPER CUP-SOKA

Super Cup: Barcelona yafugwa, Bilbao yajisafisha baada ya miaka 31

Wachezaji wa Athletic Bilbao, ambao walipata ushindi wa Super Cup ya Uhispania, Agosti 17, 2015.
Wachezaji wa Athletic Bilbao, ambao walipata ushindi wa Super Cup ya Uhispania, Agosti 17, 2015. AFP

Jumatatu jioni wiki hii, klabu ya Barcelona iliamini kua itafanya vizuri katika mechi ya marudiano lakini hadi kipenga cha mwisho ilijikuta ikiangukia pua kwa kutoka sare na klabu ya Athletic Bilbao kwa kufungana bao (1-1).

Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo yameipelekea klabu hiyo ya Barcelona kushindwa, huku Athletic Bilbao ikipata ushindi na kutwaa tuzo lao rasmi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1984, kutokana na mafanikio yao makubwa katika mechi ya awali ambapo ilipata ushindi wa mabo (4-0) dhidi ya Barcelona.

Hakukuwa na miujiza kwa Barcelona, ambayo hata hivyo iliimarisha matumaini kufuatia bao liliowekwa kimyani na Lionel Messi katika dakika ya (44) kabla ya mapumziko. Lakini kufukuzwa kwa Gerard Piqué katika dakika ya 56, Athletic Bilbao ilikuja juu na kusawazisha kupitia mchezaji wake Aritz Adurizkatika dakika ya (74).

Hakukua na maajabu yoyote, au miujiza yoyote kwa klabu ya Barcelona ambayo iliikua mshindi katika michuano ya Liga-Cup, katika michuano ya ligi ya Mabingwa na kisha katika michuano ya Super Cup ya Ulaya Jumanne iliyopita. Barcelona imekosa nafasi ya kujazia tuzo ilizozipata mwaka 2009. Vijana wa Luis Enrique bado wanaweza kumudu mara tano kama watafanikiwa kupata ushindi wa michuano ya Kombe la Dunia la klabu Bingwa itakayochezwa mwezi Desemba.

Ni furaha tele kwa klabu ya Athletic Bilbao kwa kujipatia ushindi na kutwaa tuzo hilo la Sper Cup, baada ya klabu hii kupoteza sifa ya kujinyakulia tuzo hilo miaka 31 iliyopita. Kwa miongo mitatu ambayo Athletic Bilbao walikuwa wakisubiri kuweza uleta matumaini kwa mashabiki wao.