Twiga Stars, Harambee Starlets-Soka

Twiga Stars na Harambee Starlets zatoka sare ya 1-1

Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Tanzania.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Tanzania.

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars, ililazimisha sare ya bao 1 kwa 1 na Harambee Starlets ya Kenya katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita visiwani Zanzibar.

Matangazo ya kibiashara

Starlets ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza kupitia Tabatha Chacha na baadaye Twiga Stars kusawazisha katika kipindi cha pili kwa kufunga penalti iliyotiwa kimyani na Asha Rashid.

Mchuano huu ulikuwa muhimu kwa Twiga Stars ambao wamepiga kambi Zanzibar kujiandaa kwa michuano ya Afrika itakayoanza mwezi ujao jijini Brazaville nchini Congo.

Kenya walishindwa kufuzu lakini walitumia mchuano huo kuendelea kujiweka katika hali nzuri kwa mashindano yajayo.

Tanzania ambayo itakuwa ikishiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza, itajumuika na wenyeji wao Congo Brazaville, Ivory Coast, Nigeria ambao wamecheza mara 2, sawa na Cameroon.

Mataifa mengine ni pamoja na Afrika Kusini, Misri na Ghana.