FIFA-SOKA

Jérôme Valcke aachishwa kazi

Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Jérôme Valcke, katika mkutano na waandishi wa habari, Zurich, Uswisi, Mchi 1, 2014.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Jérôme Valcke, katika mkutano na waandishi wa habari, Zurich, Uswisi, Mchi 1, 2014. Reuters/Arnd Wiegmann

Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka duniani FIFA Jérôme Valcke amesimamishwa kazi kwa tuhma za ufisadi.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii unakuja baada ya tuhma za Valcke mwenye umri wa miaka 54 na raia wa Ufaransa kutuhumiwa kuuza tiketi za kuingia katika michuano ya kombe la dunia kwa bei ya juu katika michuano ya kombe ya dunia.

Valcke ambye amekuwa katika wadhifa huo tangu mwaka 2007 amekanusha madai hayo na kusema ni mbinu za kumharibia jina baada ya kuonesha nia ya kuwania urais wa Shirikisho hilo.

Tuhma za ufisadi zimekuwa zikiwaumiza viongozi wa soka duniani akiwemo rais Sepp Blatter ambaye ameitisha uchaguzi mpya wa Shirikisho hilo mapema mwaka ujao.

Wiki hii viongozi wa mashtaka nchini Uswizi walikubali kuwasafirsuha maafisa 14 wa FIFA wanaoshiiliwa kwenda kufungiliwa mashtaka ya ufisadi nchini Marekani.