Gor Mahia mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Kenya

Sauti 21:57
Wachezaji wa Gor Mahia wakisherehekea goli
Wachezaji wa Gor Mahia wakisherehekea goli

Klabu ya soka ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya kwa mwaka wa tatu mfululizo imenyakua taji la  ligi kuu ya soka nchini humo KPL.Licha ya mazingira magumu ya ukosefu wa mfadhili, klabu hii maarufu kwa jina la Kogalo yenye makao yake jijini Nairobi, imedhirisha kuwa ndio bora baada ya kunyakua taji hilo bila hata kufungwa hata mchuano mmoja.Ndio mada yetu Jumapili hii.Tunaizungumzia Gor Mahia.