Pata taarifa kuu
SOKA-KENYA

Gor Mahia watwaa taji la ligi kuu nchini Kenya bila kufungwa

Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Kenya Gor Mahia
Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Kenya Gor Mahia
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
Dakika 2

Klabu ya Gor Mahia imekabidhiwa rasmi taji la ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini humo msimu huu wa mwaka 2015.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kukamilika rasmi kwa ligi kuu ya soka nchini humo siku ya Jumapili jioni baada ya michuano ya mwisho.

Gor Mahia imemaliza vizuri msimu huu kwa kupata ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Muhoroni Youth mchuano uliochezwa katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Klabu hiyo ambayo inanyakua ubingwa huu mara tatu mfululizo mwaka 2013, 2014 na sasa mwaka 2015 haijafungwa hata mchuano mmoja katika michuano 30 iliyocheza.

Msimu huu, Gor Mahia wameshinda mechi 24 na kwenda sare michuano sita na kufunga mabao 60 na kumaliza ligi hiyo kwa alama 78.

Nafasi ya pili imechukuliwa na mabingwa wa zamani wanajeshi Ulinzi Stars kwa alama 58 huku nafasi ya tatu ikiwaendea Sofapaka FC kwa alama 47.

Watani wa jadi wa Gor Mahia, AFC Leopards nao wamemaliza katika nafasi ya saba kwa alama 41 huku wawakilishi wa eneo la Pwani Bandari FC wakimaliza katika nafasi ya nne kwa alama 46.

Vlabu vya KCB na Nakuru All Stars vimeshushwa daraja msimu huu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.