FIFA-SOKA

FIFA yakataa rufaa ya Platini kuhusu kusimamishwa kwake

Michel Platini Mei 2015 katika mkutano wa FIFA, Zurich.
Michel Platini Mei 2015 katika mkutano wa FIFA, Zurich. AFP PHOTO / FABRICE COFFRIN

Jumatano Novemba 2015, Bodi ya rufaa ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) imefutilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Joseph Blatter pamoja na Michel Platini kwa ajili ya kusimamishwa kwao siku 90.

Matangazo ya kibiashara

FIFA imethibitisha adhabu ya Kamati ya Nidhamu na Maadili iliyochukua dhidi ya rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya, pamoja na Uswisi ambaye ni rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA).

Habari mbaya kwa Michel Platini. Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) limethibitisha Jumatano hii Novemba 18 kusimamishwa Michel Platini kwa muda wa siku 90. Michel Platini, anayetuhumiwa kupokea Euro milioni 1.8 katika mazingira ya kutatanisha mwaka 2011, amejikuta Jumatano wiki hii rufaa yake inakataliwa na Kamati ya rufaa ya FIFA.

Rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) si peke yake anayehusishwa katika kesi hii. Joseph Blatter, rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), pia amejikuta rufaa yake haipokelewi. Joseph Spp Blatter pia alisimamishwa hadi Januari 5, 2016 kwa kwa kutoa pesa hiyo kwaMichel Platini.

"Uamuzi huu si mshangao"

"Uamuzi huu si mshangao", wanasheria wa Michel Platini wamesema katika taarifa yao. "Uamzi huu ulikua ukisubiriwa na Michel Platini pamoja na wanasheria wake. Uamzi huu unathibitisha kwamba FIFA, kupitia taasisi zake za ndani, inaendesha kampeni dhidi ya Michel Platini kwa ukiukwaji wa haki za upande wa utetezi. "

Tangazo hilo pia linapunguza hata hivyo uwezekano wa Michel Platini kuwania nafasi ya urais wa FIFA, Februari 26, 2016. Faili ya kugombea kwa mwanasoka wa zamani, ambaye alipewa nafasi kubwa ya kuwa rais wa FIFA kabla ya kukutuhumiwa kosa hilo haitajadiliwa.