LIGI YA MABINGWA-SOKA-UEFA

Kilio cha Man Utd kwa kuondolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya

Manchester United wameangukia pua baada ya kufungwa Jumanne hii na Wolfsburg kutoka Ujerumani kwa mabao 3-2, na hivyo kuaga Ligi ya Klabu Bingwa barani Ulaya.

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal.
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal. DR
Matangazo ya kibiashara

Vijana hao wa Louis van Gaal walijikuata hadi kipenga cha mwisho wakibwagizwa mabao 3-2, licha ya kuwa na matuamaini ya kushinda ugenini.

Manchester United walianza vizuri baada ya Anthony Martial kuwafungia bao la kwanza alipopata pasi kutoka kwa Juan Mata.

Hata hivyo Wolfsburg walikuja juu na kusawazisha katika dakika tatu baadaye kupitia mchezaji wa kiungo. Bao la pili la Wolfsburg liliwekwa kimyani na Vieirinha, na hivyo kuwaziba domo Manchester na mashabiki wake.

Katika harakati za za kulinda lango la Wolfsburg, Josuha Guilavogui alijikuta amejifunga, na hivyo kupelekea Manchester United kuwa na matiumaini ya kusonga mbele, lakini hadi kipenga cha mwisho walijikuta wamebamizwa mabao 3-2.

Katika mechi nyingine iliyozikutanisha klabu za CSKA kutoka Urusi na PSV Eindhoven. PSV Eindhoven waliibuka mshindi wa mabao 2-1.

Wakati huo huo Paris St Germain iliiburusa Shakhtar Donetsk kwa mabao 2-0.
Nayo Real Madrid ikaiburuza Malmö FF kwa mabao 8-0. Sevilla iliimenya Juventus bao 1-0. B Monchengladbach ikaangukia pua kwa kufungwa na Manchester City kwa mabao 4-2. Galatasaray na FC Astana zilijikuta hadi kipenga cha mwisho zikenda ya kufungana 1-1. Benfica ilikubali kuchapwa bao 1 - 2 na Atletico Madrid.