Makocha wa vlabu vya Ulaya wakumbwa na kizungumkuti
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kocha wa klabu ya soka ya Arsenal nchini Uingereza Arsene Wenger anasema amesikishwa na uvumi kuwa kocha wa Manchester United Louis van Gaal huenda akafutwa kazi baada ya kushindwa kupata ushindi katika michuano sita iliyopita.
Kumekuwa na uvumi kuwa aliyekuwa kocha wa Chelsea aliyefutwa kazi wiki iliyopita Jose Mourhino huenda akapewa kibarua cha kuifunza Manchester United.
Wenger amesema kuwa sio jambo jema kwa yeyote kufutwa kazi kwa sababu ni jambo la huzuni sana.
Baada ya kufungwa na klabu ya Norwich mabao 2 kwa 1 mwishoni mwa juma lililopita, Vaan Gaal amesema ana wasiwasi kuhusu nafasi yake katika klabu hiyo ya Old Trafford.