CAMEROON-RWANSA-SOKA

Timu ya taifa ya soka ya Cameroon nchini Rwanda

Timu ya soka ya Cameroon yapokelewa Rwanda kushiriki katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki na Amavubi timu ya taifa ya soka ya Rwanda).
Timu ya soka ya Cameroon yapokelewa Rwanda kushiriki katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki na Amavubi timu ya taifa ya soka ya Rwanda). AFP/STR

Timu ya taifa ya soka ya Cameroon imewasili jijini Kigali nchini Rwanda kushriki katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki siku ya Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo utachezwa katika wilaya ya Rubavu, na mchuano huo ni maandalizi ya fainali za CHAN, michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani.

Mashindano haya yataanza tarehe 16 mwezi huu nchini Rwanda.

Amavubi Stars imekuwa ikipiga kambi katika wilaya ya Rubavu tangu mwisho wa mwaka uliopita kwa maandalizi ya mashindano haya.

Rwanda iko katika kundi moja na Gabon, Moroco na Cote Dvoire huku Cameroon ikiwa katika kundi la B na DRC, Angola na Ethiopia.