DRC-TP MAZEMBE-SOKA

Carteron amaliza mkataba wake na TP Mazembe

Klabu ya TP Mazembe katika fainali ya Ligi ya Mabingwa nchini Algeria, Oktoba 31, 2015.
Klabu ya TP Mazembe katika fainali ya Ligi ya Mabingwa nchini Algeria, Oktoba 31, 2015. AFP PHOTO / FAROUK BATICHE

Patrice Carteron ameondoka katika klabu ya soka ya TP Mazembe baada ya mkataba wake wa kuwa kocha kumalizika mwezi Desemba mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa klabu hiyo umetangaza rasmi kuwa umeachana na Carteron raia wa Ufaransa ambaye alijiunga na klabu hiyo yenye makao yake mjini Lubumbashi mwaka 2013 akitokea timu ya taifa ya Mali.

Kocha huyo atakumbukwa kuiongoza Mazembe kwa kunyakua ubingwa wa klabu bora barani Afrika mwaka uliopita na kuisaidia klabu hiyo kufika katika fainali ya Kombe la dunia baina ya vilabu nchini Japan mwezi Desemba mwaka jana.

Ameicha Mazembe ikiongoza msururu wa ligi kuu ya soka nchini humo.

Uongozi wa TP Mazembe sasa inamtafuta kocha mpya.