DRC-ETHIOPIA-CHAN 2016

DRC yaiburuza Ethiopia 3-0 katika Kundi B la michuano ya CHAN 2016

Kocha wa Chui wa DR Congo, Florent Ibenge.
Kocha wa Chui wa DR Congo, Florent Ibenge. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza vizuri mashindano ya soka barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza nyumbani CHAN.

Matangazo ya kibiashara

Michuano ya CHAN 2016 yalianza tangu Jumamosi hii. katika mchuano wa kwanza wa kundi B ulichezwa katika ya DRC na Ethiopia Jumapili hii, Ethiopia imepata kipigo cha mabao 3-0 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa katika mji wa Butare.

DRC ilitawala mechi hiyo iliochezwa katika mji wa Butare nchini Rwanda. Bao la kwanza la DRC liliwekwa kimyani na Guy Lisadisu katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili ya mapumziko, Heritier Luvumbu alifunga kupitia kichwa katika dakika ya 46. Nae Mechack Elia alimalizia bao la tatu dakika tisa baada ya bao la pili.

Itafahamika kwamba DRC ilishinda michuano ya CHAN mwaka 2009.

Mkwaju mmoja wazaa pointi 3

Baada ya mechi ya DRC na Ethiopia, Cameroon Angola zilijitupa uwanjani, lakini mechi hiyo haikua rahisi kwa Cameroon. Simba wa Nyika walionyesha utofauti wao dhidi ya Angola kufuatia mkwaju wa mshambuliaji Yazid Atouba, ambao ulipelekea Cameroon kuandikisha pointi 3. Hata hivyo Cameroon wamepoteza beki wao Joseph ngwen ambaye aliondolea uwanjani katika dakika ya70.

Januari 21, DRC watakutana na Angola, nao Cameroon watamenyana na Ethiopia, katika uwanja wa Huye.

Timu za Kundi B namna zinavyoshindana

1. DRC 3 pointi (+3)
2. Cameroon pointi 3 (+1)
3. Angola pointi 0 (-1)
4. Ethiopia pointi 0 (-3)