REAL MADRID-SPORTING GIJON

Liga: Real Madrid yatamba dhidi ya Sporting Gijón

Pamoja na Zidane, kwa sasa, Real Madrid imeanza kufanya vizuri katika michuano yake miwili ambayo imeshacheza katika kipindi kisichozidi wiki mbili.

Cristiano Ronaldo , nyota wa Real Madrid aliyefunga mabao mawili dhidi ya Sporting Gijón.
Cristiano Ronaldo , nyota wa Real Madrid aliyefunga mabao mawili dhidi ya Sporting Gijón. REUTERS/Juan Medina
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mechi ya awali kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Deportivo La Corogne wiki iliyopita, Real Madrid imepata ushindi wa pili Jumapili hii katika uwanja wa mpira wa Bernabeu, ambapo imecheza na klabu mbovu ya Sporting Gijón.

Mechi hii ambayo imechezwa hasa katika kipindi cha kwanza katika hali ya kikiri kakara, Real Madrid iliongoza kipindi hiki kwa mabao 5-1. Lakini mabao 4 yameingizwa katika muda wa dakika zisiyozidi 20 tangua kuanza kwa kipindi cha kwanza. Ronaldo ameifungia klabu yake mabao mawili. Bao la tatu limewekwa kimyani na Bale na la nne limewekwa wavuni na Benzema. Bao la tano limeingizwa kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika

Hata hivyo Sporting Gijón imekuja juu na kufunga bao moja la kufuta machozi, bao lililofungwa na Isma Lopez.

Real watabasamu

Kwa sasa Real Madrid wamekua na matumaini ya kusonga mbele ikilinganishwa na wakati wa enzi za Benitez. Kwa muda usiozidi wiki moja Real Madrid imepata ushindi mara mbili chini ya usimamizi wa Zinedine Zidane.

Sporting Gijón inachukua nafasi ya 18 katika ligi kuu ya Uhispania (La Liga) baada ya kushindwa mara saba katika mechi 8 ziliyopita.

Pointi mbili mbaya upande wa Real

Licha ya ushindi, si kila kitu kilikuwa kimekamilika upande wa Real Madrid. Kuondoka uwanjani kwa Gareth Bale na Karim Benzema baada ya kupata majeraha kulisababisha klabu hii ya Real Madrid kudhoofika kidogo upande wa washambuliaji. Kinachosalia ni kujua iwapo majeraha haya ni makubwa. Kinachofahamika tu ni kwamba katika kipindi cha pili Real Madrid haikuonyesha mchezo mzuri, licha ya kuongoza kwa ushindi wa mabao 5-1 hadi kipenga cha mwisho.