CHAN-GUINEA-TUNISIA-SOKA

Guinea na Tunisia zatoka sare ya kufungana 2-2

Ahmed Akaichi aliyeifungia Tunisia mabao mawili katika mchuano wake na Guinea katika michuano ya CHAN inayoendelea Rwanda..
Ahmed Akaichi aliyeifungia Tunisia mabao mawili katika mchuano wake na Guinea katika michuano ya CHAN inayoendelea Rwanda.. AFP PHOTO / CARL DE SOUZA

Timu ya taifa ya soka ya Guinea inayoshiriki katika michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN inayoendelea nchini Rwanda, ilitoka nyuma na kusawazisha mabao 2 waliyokuwa wamefungwa na Tunisia katika mchuano wa Kundi C.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo uliochezwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali ulimalizika kwa timu zote mbili kufungana mabao 2 kwa 2.

Tunisia ilianza kupata bao katika dakika ya 33 kipindi cha kwanza na Ahmed Akaïchi na baadaye Alseny Camara Agogo kuisawazishia Guinea katika dakika 40.

Kipindi cha pili timu zote mbili ziliendeleza mashambulizi na katika dakika ya 51, Akaichi aliifungia tena Tunisia katika dakika ya 51, huku Agogo akiisawazishia timu yake katika dakika 83.

Mchuano mwingine wa kundi hili ulizikutanisha saa moja jioni saa za Afrika ya Kati Niger na Nigeria.

Timu za Kundi C namna zinavyoshindana

1. Nigeria pointi 3 (+3)
2. Guinea pointi1 (0)
3. Tunisia pointi 1 (0)
4. Niger pointi 9 (-3)

Jumnne hii, itakuwa ni zamu ya kundi la D, Zimbabwe itachuana na Zambia, na baadaye Mali watamenyana na Uganda.

Mechi hizi zitapigwa katika uwanja wa Umuganda katika mji wa Gisenyi.