CHAN-MALI-UGANDA-SOKA

CHAN 2016: Mali na Uganda zatoka sare ya 2-2

Timu za Mali na Uganda zimetoka sare ya kufungana mabao 2-2 katika duru ya kwanza ya michuano ya Mataifa ya Afrika, Jumanne hii Januari 19 katika uwanja wa Rubavu. Zambia, ambao wamewafunga Zimbabwe 1-0, wamepata fursa ya kushikilia nafasi ya kwanza katika Kundi D ya michunao hii ya CHAN 2016.

Kipa wa Mali Djigui Diarra.
Kipa wa Mali Djigui Diarra. AFP PHOTO / MARTY MELVILLE
Matangazo ya kibiashara

Makala haya ya nne ya Michunao ya Mataifa inakwenda vizuri, ambapo katika mechi 8 mabao 19 ndio yameingzwa nyavuni. Timu za Mali na Uganda zimechangia katika burudani hii kwa sare ya mabao 2-2 katika uwanja wa Rubavu, Jumanne hii Januari 19, katika duru ya kwanza ya michuano ya CHAN 2016.

Uganda wameanza kuliona lango la Mali kupitia mpira wa kichwa wa Erisa Ssekisambu, ambaye alipata fursa hiyo ya kuandikisha bao la kwanza dhidi ya Mali katika dakika ya 12 ya mchezo (0-1, 12). Mali walikuja juu na kusawazisha kwa mkwaju uliopigwa na Sekou Koita (1-1) katika dakika ya 24.

Uganda imeingiza bao la pili baada ya muamuzi kuidhabu Mali, na kutengwa mkwaju wa penalti, bao ambalo limeingizwa na Faruku Miya, nahodha wa Uganda, na hivyo kuandikisha bao la 2-1 katika dakika ya 41. Hata hivyo mashabiki wa timu ya Mali wamemlaumu muamuzi kwamba alijidanganya kwa kutoa penalti hiyo, kwani hakuna madhambi ambayo yalitendwa na mchezaji wao.

Mapema katika kipindi cha pili, Mali ilikuja juu na kutawala mpira, hadi katika dakika ya 48, kupitia mchezaji wake Hamidou Sinayoko ilisawazisha. Hadi kipenga cha mwisho Mali na Uganda walijikuta wanatoka sare ya mabao 2-2.

Mapema siku Siku ya Jumanne, timu ya Zambia imeiadhibu Zimbabwe bao 1-0, kupitia mchezaji wake Isaka Chansa , katika dakika ya 58.

Mali itakutana na Zimbabwe Januari 23 katika uwanja wa Rubavu, wakati ambapo mechi nyingine katika kundi D itazikutanisha Uganda na Zambia.

CHAN 2016: Timu za kundi D namna zinavyoshindana

1. Zambia pointi 3 (+1)
2. Mali 1pointi (0)
- Uganda pointi 1 (0)
4. Zimbabwe pointi 0 (-1)