RWANDA-GABON-CHAN 2016

CHAN 2016: Rwanda yafuzu robo fainali baada ya kuibwaga Gabon

Rwanda ni timu ya kwanza kufuzu robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika CHAN 2016. Rwanda wenyeji wa michunao ya CHAN 2016, wana uhakika wa kumaliza wa kwanza au wa pili katika Kundi A.

Timu ya taifa ya Rwanda, Novemba 2015.
Timu ya taifa ya Rwanda, Novemba 2015. AFP PHOTO / SALAH LAHBIBI
Matangazo ya kibiashara

Rwanda imegaragaza Gabon kwa mabao 2-1, Jumatano hii Januari 20 katika uwanaja wa Amahoro mjini Kigali, huku ikiwa hatarini Gabon baada ya kutofanya vizuri katika mechi mbili ambazo imeshacheza.

Lengo limefikiwa kwa asilimia 50 kwa wenyeji Rwanda, baada ya kuifunga Gabon na kufuzu kwa robo fainali. Rwanda wana uhakika wa kumaliza angalau wa pili katika Kundi A.

Ushindi huu wa mabao mawili, Amavubi au Manyigu, jina la utani la timu ya taifa ya Rwanda imeupata kupitia mchezaji wake mahiri Ernest Sugira. Bao la kwanza liliingizwa katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza na bao la pili katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili.

Ulinzi wa Gabon watiliwa shaka

Katika dakika ya 42, Jacques Tuyisenge aliangushwa katika eneo la hatari la Gabon, ambapo wengi walidhani kuwa kuwa utapigwa mkwaju wa penalti lakini haikua hivo. Mchezo uliendelea. Hata hivo, Ernest Sugira alilisakama lango la Gabon na kujikuta anafaulu kuipatishia timu yake bao la kwanza katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.

Baada tu ya mapumziko, namba 16 wa Gabon akapigilia msumari, baada ya mpira kumcheza, alipokua anataka kuokoa jahazi, akajikuta mpira unaingizwa wavuni na Ernest Sugira: 2-0.

Côte d’Ivoire yaiburuza Morocco 1-0

Kwa upande mwengine timu ya Côte d’Ivoire imeifunga Morocco bao 1-0 katika duru ya kwanza ya michuano ya Mataifa ya Afrika Jumatano hii Januari 20 mjini Kigali. Matokeo ambayo yanaiweka kwa muda Côte d’Ivoire kwenye nafasi ya pili katika Kundi A (nyuma ya Rwanda ambayo tayari imefuzu kwa robo fainali).

Rwanda inajiandaa katika mechi ifuatayo kucheza na Morocco, huku Gabon ikijiandaa kumenyana na Côte d’Ivoire Januri 24, 2016.

CHAN 2016: Timu za kundi A namna zinavyoshindana

1. Rwanda pointi 6 (+2)
2. Côte d’Ivoire pointi 3 (0)
3. Morocco pointi 1 (-1)
- Gabon pointi 1 (-1)