DRC-ANGOLA-CHAN 2016

CHAN 2016: DRC yauona mlango wa robo fainali

Mchezaji wa DRC Joël Kimwaki.
Mchezaji wa DRC Joël Kimwaki. AFP PHOTO / CARL DE SOUZA

Timu ya DRC imeanza kuwa na uhakika wa kuona mlango wa robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika CHAN 2016, kufuatia ushindi wake, Alhamisi hii Januari 21, wa mabao 4-2 dhidi ya Angola, katika uwanja wa Huye.

Matangazo ya kibiashara

Lakini bado mashabiki wa timu hii wana wasi wasi kuwa huenda DRC ikabanduliwa bila kuona mlango huo.

Timu ya DR Congo imeonyesha mchezo mzuri dhidi ya Angola na kwa sasa inaishinda mabao 3-1, katika Kundi B la michuano ya CHAN  2016.

DRC imewashangaza wengi hasa mashabiki wake waliokuwepo katika uwanja wa mpira wa Huye. Katika dakika ya 8 ya mchezo, kiungo wa kati Neslon Munganga alifunga bao la kwanza katika mazingira ya kutatanisha. Kipa wa Angola Landu Mavanga alishindwa kuzuia mpira uliopigwa kutoka kwenye pembe la uwanja, baada ya beki wa timu hiyo kutoa mpira nje ya uwanja. Mshangao mkubwa ni kwamba mpira ulizunguka kwenye mgongo wa kipa Landu Mavanga, na hatimaye Neslon Munganga akamalizia kwa kupachika bao la kwanza: 1-0.

Bao la pili liliingizwa na Mechak Elia katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza.

DRC ilikuja juu na kutawala mpira, hadi dakika ya dakika ya 38 ambapo Mavanga alijikuta akifungwa bao la tatu na mchezaji Jonathan Bolingi: 3-0.

Katika kipindi cha pili Angola walikuja juu. Katika dakika ya 78, Gelson aliipatishia timu yake bao la kwanza, na hivo kupunguza idadi ya mabao: 3-1. Katika dakika ya 82, beki Joel Kimwaki alijifunga bao: 4-2. Alitaka kuzuia mkwaju wa Manucho, lakini akajikuta amejifunga.

Lakini kabla ya beki wa DRC kujifunga bao katika dakika ya 82, kiungo wa kati wa DRC Merveille Bope alikuwa ameifungia timu yake bao la nne katika dakika ya 81: 4-1.

DRC itaondolewa katika michuano ya CHAN 2016 iwapo Ethiopia wataifunga Cameroon katika mchezo wao Alhamisi hii jioni, Januari 21, kisha Angola Januari 25, na kwamba Cameroon waiburuze Leopards katika siku nne zijazo. Hali yoyote yawezekana.