VALENCIA-BARCELONA-NEVILLE

NEVILLE: Hatustahili kufungwa magoli mengi kiasi hiki, licha ya kuwa Barcelona ni timu bora duniani

Kocha mkuu wa klabu ya Valencia, Gary Neville
Kocha mkuu wa klabu ya Valencia, Gary Neville Valencia FC

Kocha mkuu wa klabu ya Valencia ya nchini Uhispania, muingereza, Gary Neville amesema kuwa kushuhudia timu yake ikifungwa magoli 7 na FB Barcelona katika dimba la Nou Camp ilikuwa ni kitu kibaya zaidi kukishuhudia kwenye mpira wa miguu.

Matangazo ya kibiashara

Kupoteza mchezo wa Jumatano kwenye nusu fainali ya michuano ya kombe la Copa del Rey, kumeongeza shinikizo zaidi kwa Neville ambaye toka amechukua timu hiyo, imecheza mechi takriban 8 za ligi bila kupata ushindi.

Punde mara baada ya kumalizika kwa mtanange wenyewe, Neville aliwaambia waandishi wa habari kuwa usiku wa jana usingekuwa mzuri kwake na alitarajia kutokupata usingizi, ambapo akasisitiza kuwa hatang'atuka kwenye kibarua chake.

Neville amesema kipigo cha Jumatano, ni kipigo kibaya zaidi ambacho amekumbana nacho katika kipindi chote alichocheza.

Baada ya mechi kumalizika pia, mitandao ya kijamii ilikuwa bize wakati wote, huku kwenye mtandao wa Twitter mashabiki wakiandika neno #Nevilleveteya ambalo maana yake ni Neville ondoka sasa, lilisambazwa na mashabiki wengi wa Valencia.

Lionel Messi akiwa na mchezaji mwenzake Neymar da Silva
Lionel Messi akiwa na mchezaji mwenzake Neymar da Silva REUTERS/Stringer EDITORIAL USE ONLY

Kocha huyo ameongeza kuwa awali alikuwa haamini kama ingetokea katika kipindi cha miaka 18 na akarudia kusisitiza uungwaji mkono anaoupata toka kwa bodi ya klabu hiyo na kwaamba alishajenga mazingira ya uvumilivu.

Redio moja ya Uhispania, imeripoti kuwa mmiliki wa klabu hiyo, Peter Lim ataamua mustakabali wa Neville katika saa chache zijazo.

Kwenye mtanange huo, mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez ndiye aliyekuwa mwimba mkali kwa Valencia baada ya kutumbukiza mpira kwenye nyavu za timu hiyo mara nne, huku mchazji bora wa dunia Lionel Messi yeye aifunga mabao matatu "Hat-trick" na kumuacha Neville akipata ushindi mara nne katika mechi za kombe la mfalme.

Valencia nasafiri kucheza na Real Betis siku ya Jumapili ya wiki hii, ikiwa kwenye nafasi ya 12 alama tano tu na mstari wa timu zinazokaribia kushuka daraja.

Neville amesema anajisikia vibaya kuwaangusha mashabiki wa timu hiyo ambao amesema hawakustahili aibu waliyoipta toka kwa moja ya timu bira duniani, na yenye wachezaji wa kiwango cha juu kwa sasa.

Mkurugenzi wa ufundi wa Valencia, Jesus Gracia Pitarch ameeleza kipigo cha Jumatano kama kipigo kibaya zaidi katika historia ya timu yao.