Michezo - Barcelona

Lionel Messi arejea mazoezini

Lionel Messi akisherehekea moja miongoni mwa mabao yake akiwa pamoja na mchezaji mwenzie Neymar
Lionel Messi akisherehekea moja miongoni mwa mabao yake akiwa pamoja na mchezaji mwenzie Neymar Reuters/Albert Gea

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na Clubu ya Barcelona ya Uhispania, Lionel Messi amerejea mazoezini alhamisi hii katika timu yake ya Barcelona baada ya kupewa matibabu kwa kusumbuliwa na tatizo la mawe kwenye figo, hali ambayo ilimsababishia kutoshiriki kwake katika mashindano ya kombe la dunia ya vilabu mwezi Desemba mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka katika Clabu ya Barcelona zinaeleza kwamba Nyota wa Argentina amefanya vipimo ili kutathimini hali yake ya afya.

Messi alikosa mechi ya nusu fainali ya pili siku Jumatano kombe la Mfalme na Club ya Valencia, ambapo Barcelona ilishinda jumla ya mabao 8 kwa moja baada ya fainali ya kwanza timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Mchezaji jhuyo bora duniani atashuhudiwa uwanjani siku ya Jumapili katika mecho ya kigi kuu nchin Uhispania ambapo Barcelna itapepetana na Celta Vigo katika uwanja wa Camp Nou ambapo anahitaji mabao mawili tu kuwa mchezaji wa kwanza katika Ligi ya Hispania kutimiza mabao 300.

wakati hali ya mchezaji huyo wa Kimataifa ikirejea kuwa shwari kama ilivyokuwa hapo awali, clubu yake ya Barcelona imeanza kujipanga katika mchezo wake wa ligi kuu.