PSG-AURIER-SOKA

PSG: Aurier asikilizwa na Uongozi wa klabu

Serge Aurier na Laurent Blanc wakati wa kikao cha mafunzo katika uwanja wa Saint-Germain-en-Laye Aprili 14, 2015.
Serge Aurier na Laurent Blanc wakati wa kikao cha mafunzo katika uwanja wa Saint-Germain-en-Laye Aprili 14, 2015. AFP/AFP

Mchezaji wa kimataifa wa Paris SG Serge kutoka Côte d’Ivoire, Serge Aurier, ambaye alichukuliwa vikwazo vya kusimamishwa katika klabu hiyo kwa wiki moja sasa kutokana na utovu wake wa nidhamu, "amejibu maswali ya Uongozi wa klabu yake," PSG imesema Jumatatu hii jioni katika tovuti yake.

Matangazo ya kibiashara

"Jumatatu hii saa tano mchana, Serge Aurier amepokelewa katika makao makuu ya Paris Saint-Germain na Olivier Létang, Naibu Mkurugenzi wa mchezo pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimali watui," PSG imeandika katika taarifa yake.

Mchezaji "amejibu maswali ya uongozi kufuatia maneno aliotoa na kurusha hewani kwenye mtandao wa kijamii, katika usiku wa Februari 13 na14. Kufuatia mahojiano haya, Uongozi wa Paris Saint-Germain utamtaarifu mchezaji uamuzi kwa wakati mwafaka. "

"Kabla ya tarehe hiyo, klabu haitazungumzia kuhusu kesi hii," klabu hii imeonya. Waandishi wa habari, waliokuwepo Jumatatu hii katika makao makuu ya Paris SG katika mji wa Boulogne-Billancourt (kitongoji cha mji wa Paris), hawakuweza kumuona Aurier, lakini waliona tu gari nyeusi yenye vio vyeusi ikiwasili na kuondoka katika jengo hilo ambako ni makao makuu ya PSG.

Aurier alichukuliwa vikwazo vya kusimamishwa Jumapili, Februari 14 licha ya kuomba msamaha, hasa baada ya kumtusi kocha wake Laurent Blanc kuwa ni "mjinga" katika mazungumzo ya video pamoja na watumiaji wa intaneti, katika usiku uliofuata.