FIFA-BLATTER-PLATINI-UFISADI

FIFA: adhabu dhidi ya Blatter na Platini yapunguzwa kutoka miaka 8 hadi 6

Rais wa Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) anayemaliza muda wake Joseph Blatter na Rais wa UEFA Michel Platini wamejikuta adhabu waliopewa imepunguzwa kutoka miaka 8 hadi 6. Uamuzi huu umetangazwa Jumatano hii na Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA), baada ya wawili hawa kukata rufaa.

Rais wa UEFA Michel Platini (kulia) na Rais wa FIFA Sepp Blatter baada ya uchaguzi wa kiongozi huyu wa FIFA, katika Mkutano mkuu wa FIFA, mjini Zurich, Mei 29, 2015.
Rais wa UEFA Michel Platini (kulia) na Rais wa FIFA Sepp Blatter baada ya uchaguzi wa kiongozi huyu wa FIFA, katika Mkutano mkuu wa FIFA, mjini Zurich, Mei 29, 2015. REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati wagombea wawili kwenye nafasi ya urais wa FIFA wamebaini, zikisalia tu siku mbili za uchaguzi wa rais wa taasisi hiyo, kwamba waibuka washindi.

Kamati ya rufaa ya FIFA haikutoa uamzi mzuri kwa Blatter na Platini wanaoadhibiwa kwa sababu ya malipo yenye utata wa Euro milioni 1.8, ziliotolewa na Blatter akimlipaPlatini mwaka 2011 kwa ajili ya kazi ya kushauriana iliyomalizika tangu mwaka 2002. Kamati hiyo imebaini kwamba wawili hawa wamekutwa na hatia ya kukiuka Ibara nne za maadili ya sheria na wamekutwa hasa na hatia ya mgogoro wa kimaslahi.

Wakati huo huo, Tume hiyo imefutilia mbali madai ya "rushwa" na kufuta rufaa ya kitengo cha uchunguzi cha FIFA ambacho kiliomba Joseph Blatter na Michel Platini wasimamishwe maisha katika shughuli zote zinazohusiana na soka.

Kwa sasa wawili hawa hawana tena matumani ya kufutiwa makosa yanayowakabili, kazi kubwa imebaki kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (TAS), ambayo ni Mahakama ya ngazi ya juu katika michezo.

Uamuzi huo mpya wa FIFA ni pigo kubwa kwa Michel Platini, ambae tayari amelazimishwa kuachana kuwania katika kinyan'ganiro cha urais wa FIFA, ambapo alikua amepewa nafasi kubwa ya kumrithi Joseph Blatter. Kwa sasa nafasi ambayo itamuwea rahisi huenda kuwani ni ile ya Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).

Joseph Blatter na Michel Platini waliosimamishwa kwa kipindi cha miaka 8 katika shughuli zote zinazohusiana na soka kutokana na malipo ya Euro milioni 1.8 walikua wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya maadili ya FIFA uliotangazwa Desemba mwaka 2015.