Messi aipatia ushindi Barcelona dhidi ya Arsenal
Katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa mtoano wa timu 16 wa klabu bingwa barani Ulaya (UEFA), Barcelona imefanikiwa kuiadhibu Arsenal kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza ulichezwa Jumanne hii katika uwanja wa Emirates.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mchezaji Nyota wa klabu hiyo Lionel Messi alifaanikiwa kuishindia klabu yake mabao mawili. Bao la kwanza liliwekwa kimyani katika dakika ya 71, huku bao la pili likingizwa katika dakika ya 83. Bao hili a pili lilifungwa kwa njia ya penalti.
Wakati huo huo Juventus imetoka sare na Bayern Munich ya kufungana 2-2. Bayern imeshindwa kufanya vizuri ikiwa nyumbani.
Itafahamika kwamba katika mchezo huo klabu ya Bayern Munich ndio ilianza kuliona lango la Juventus, baada ya mchezaji Thomas Muller kuuweka mpira wavuni katika dakika ya 43 kipindi cha kwanza. Bao la pili lilifungwa na Arjen Robben katika dakika ya 55 kipindi cha pili.
Hata hivyo Juventus licha ya kufungwa mabao hayo mawili hawakukatika nguvu, waliendelea kuonyesha mchezo mzuri, na katika dakika ya 63 kipindi cha pili Paulo Dybala aliiandikishia klabu yake bao la kwanza, huku Stefano Sturaro akiandika bao la pili la kusawazisha katika dakika ya 76.
Leo Jumatano kutachezwa mechi 2, Dynamo Kiev wakiwa nymbani watawapokea Man City nchini Ukraine na PSV Eindhoven pia wakiwa nyumbani watamenyana dhidi ya Atletico Madrid.