Jukwaa la Michezo

Gianni Infantino achaguliwa rais mpya wa FIFA

Sauti 23:38
Gianni Infantino rais mpya wa FIFA
Gianni Infantino rais mpya wa FIFA

Gianni Infantino amechaguliwa rais mpya wa Shirikisho la soka duniani FIFA.Infantino mwenye umri wa miaka 45, raia wa Uswizi na mwenye asili ya Italia alimshinda Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, kwa kupata kura 115 dhidi ya 88 alizopata Al Khalifa.Rais huyu  mpya anachukua nafasi ya Sepp Blatter aliyejiuzulu mwaka uliopita kwa sababu za ufisadi.