CHELSEA-NORWICH-EPL-SOKA

Norwich washindwa kufanya vizuri dhidi ya Chelsea

Diego Costa mchezaji wa Chelsea akisheherekea bao lake dhidi ya Swansea.
Diego Costa mchezaji wa Chelsea akisheherekea bao lake dhidi ya Swansea. REUTERS/Toby Melville

Norwich wameangukia pua wakiwa nyumbani Carrow Road, baada ya kufungwa na Chelsea kwa mabao 2-1, na hivo kujikuta katika eneo la hatari Ligi ya Premia.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo yameifanya Chelsea chini ya meneja wao Guus Hiddink, kuendelea kupanda kileleni, huku Norwich ikijikuta katika eneo la hatari, na bado inaendelea kupoteza katika ligi hii ya Premia.

Mabao ya Chelsea yameingizwa na wachezaji Blues Kenedy na Diego Costa. Bao la kwanza limeingizwa na Beki wa Blues Kenedy katika sekunde 39 baada ya mchezo kuanza. Bao la pili limewekwa kimyani na Diego Costa, sekunde chache kabla ya mapumziko. Hata hivyo mashabiki wengi wa soka wanasema kuwa bao la Diego Costa si halali kwanii alionekana kuotea.

Hata hivyo Norwich ilikuja juu, lakini waliambulia pa tupu, licha ya Nathan Redmond kuipatishia timu yake bao la kufuta machozi,. Lakini kabla ya bao hilo, Cameron Jerome alikosea kuliona lango la Chelsea baada ya mpira aliocheza kugonga mwamba wa goli. Hadi kipenga cha mwisha Norwich ilijikuta ikiangukia pua kwa kufungwa mabao 2-1. Na mechi hii ni ya nane kati ya tisa ambazo Norwich imeshindwa kufanya vizuri.

Chelsea, kufuatia matokeo hayo wamepanda nafasi ya nane, huku Norwich wakijikuta kwenye mstari mwekundu.

Kwa sasa Norwich wanajianda kukutana na Swansea, ambvayo inaongoza kwa alama tatu mbele yao, huku Chelsea wakiikaribisha nyumbani Stoke Jumamosi.

Katika mechi zingine za EPL zilizochezwa Jumanne hii ni pamoja na Sunderland kutoka sare na Crystal Palace ya kufungana 2-2, Leicester kutoka sare na West Brom ya kufungana 2-2, Bournemouth kuifunga Southampton 2-0 na Everton kuifunga Aston Villa 3-1.