MANCHESTER UNITED-LIVERPOOL-SOKA

Manchester United yaangukia pua

Wachezaji wa Liverpool Steven Gerrard (kushoto) na Mamadou Sakho (kulia) Anfield, Aprili 27, 2014.
Wachezaji wa Liverpool Steven Gerrard (kushoto) na Mamadou Sakho (kulia) Anfield, Aprili 27, 2014. REUTERS/Darren Staples

Nchini Uingereza, mwishoni mwa wiki hii iliyopita kulishuhudiwa mechi mbili zilizochezwa katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Manchester United wameangukia pua kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 na West Bromwich Albion, bao lililofungwa na Solomon Rondon. Hata hivyo kiungo Juan Mata alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Nao Liverpool wakichezea ugenini kwenye uwanja wa Selhurst Park waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace.

Crystal Palace ndio walianza kuandika bao la kwanza kwa bao la Joe Ledley kisha Liverpool wakasawazisha na kubadii matokeo ya awali ya mchezo huo kwa kuingiza bao la kwanza kupitia mshambuliaji wake Roberto Frimino. Naye Christian Benteke aliipatishia timu yake ushindi kwa bao la mkwaju wa penati. Bao hili la pili limeingizwa katika dakika za lala salama.

Hayo yakijiri klabu ya Leicester hadi Jumatau hii Machi 7, inaongoza katika michuano ya ligi ya EPL kwa alama 60, mabao 21 katika mechi 29. Tottenham inachukua nafasi ya pili kwa alama 55, mabao 27 katika mechi 29. Aston Villa inaburura mkia kwa alama 16, mabao iliyoingizwa 33 katika mechi 29.