PSG-TROYES-SOKA

Ligi kuu: PSG, mabingwa wa rekodi

Wachezaji wa PSG wakisheherekea taji lao la sita la ubingwa mabingwa wa Ufaransakatika uwanja wa Troyes, iliofungwa mabao 9-0 Machi 13 2016.
Wachezaji wa PSG wakisheherekea taji lao la sita la ubingwa mabingwa wa Ufaransakatika uwanja wa Troyes, iliofungwa mabao 9-0 Machi 13 2016. JACQUES DEMARTHON / AFP

Baada ya ushindi wake mkubwa dhidi ya Troyes Jumapili Machi 13, Paris Saint-Germain imetangazwa rasmi mabingwa wa soka wa Ufaransa kwa mara ya nne mfululizo. PSG imepata taji la sita katika historia yake.

Matangazo ya kibiashara

Zikisalia siku nane ili kufikia mwisho wa michuano, klabu hiyo kutoka mji mkuu wa Ufaransa sasa inaweza kushiriki katika kuwania rekodi katika michuano ya ligi kuu na kujihusisha kwenye Ligi ya mabingwa, ambayo ni changamoto yake kubwa.

Paris Saint-Germain imeshinda Jumapili hii mabao 9-0 dhidi ya Troyes, timu ya mwisho katika michuano hii. PSG kwa sasa ina alama 25 mbele ya mtani wake wa jadi AS Monaco. Zikisalia tu siku nane ili michuano hiyo ifikie ukingoni, haiwezi kufikiwa kwa vile kunasalia tu alama 24 za kuchukua.

Taji hili la nne la PSG tangu klabu hii kuchukuliwa na tajiri kutoka Qatar, miaka mitano iliyopita, ilikua ikisubiriwa hata kabla ya kuanza kwa michuano hii. Kwani, kama klabu ya Paris, pamoja na wachezaji wake wa kimataifa na euro bajeti ya milioni 490, inamaliza ikiwa ya kwanza katika michuano ya ligi kuu, na ilikuwa haina mashaka. swali kuu lilikuwa: lini?

Kabla ya mwisho wa majira ya baridi, PSG ilijibu swali hili kwa kuwa mabingwa wa kwanza katika historia ya michuano ya Ligi kuu iliotabiriwa kabla ya majira ya joto.
PSG, kwa hiyo imekua bingwa katika siku 30, na hivo kupiga rekodi iliokua ikishikiliwa na Olympique Lyonnais iliotunukiwa katika siku 33 mwaka 2007 na inafanya vizuri barani Ulaya kama Bayern Munich katika Bundesliga (2013-2014).