LIGI YA MABINGWA-SOKA-UEFA

Michuano ya klabu bingwa UEFA inaendelea

Mchezaji kutoka Cote d'Ivoire Yaya Touré (kushoto) na mchezaji kutoka Argentina Sergio Aguero wakati wa ushindi wa mabao 3-1 ya Manchester City dhidi ya Dynamo Kiev.
Mchezaji kutoka Cote d'Ivoire Yaya Touré (kushoto) na mchezaji kutoka Argentina Sergio Aguero wakati wa ushindi wa mabao 3-1 ya Manchester City dhidi ya Dynamo Kiev. Reuters / John Sibley Livepic

Michuano ya klabu bingwa Ulaya inaendelea tena Jumanne hiikwa Michezo Miwili, ambapo Atletico Madrid itamenyana na Psv Endovein, huku Manchester city wakiipokea Dianamo Kiev.

Matangazo ya kibiashara

Manchester city ambao wana alama 12 watakuwa wakichezea nyumbani wakiwapokea Dianamo Kiev ya Ukraine katika uwanja wa Etihad. Dianamo Kiev ina alama 11 katika michuano hii.

Nao Atletico Madrid ambao wamewaalika nyumbani Psv Endovein watakua na kazi kubwa ya kuwaridhisha mashabiki wao ambao wanatazamiwa kumiminika uwanjani kwa wingi ili kuishangilia klabu yao. Mpaka sasa Atletico Madrid wana alama 13, nao Psv Endovein wana alama 10 katika msimamo huu.

Jumatano hii kunatazamiwa pia kuchezwa mechi mbili. Arsenal watapokelewa na Barcelona, na Bayern Munich wakimenyana na Juventus.

Fainali za Michuano inatazamiwa kuchwezwa Mei 28, 2016 katika uwanja wa San Siro Milan nchini Italy.

Itafahamika kwamba katika michuano iliopita Dynamo Kiev iliangukia pua kwa kufungwa na Man City mabao 3-1. Nao Psv Eindhovein wakiwa nyumbani walitimua vumbi na Atletico Madrid lakini hadi kipenga cha mwisho timu hizi mbili zilijikuta zikitoka sare ya kutofungana.