UGANDA-SOKA

Uganda: Micho atangaza kikosi cha wachezaji 30

Timu ya taifa ya soka ya Uganda.
Timu ya taifa ya soka ya Uganda. FADEL SENNA / AFP

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uganda Milutin Sredojevic Micho ametangaza kikosi cha wachezaji 30 kitakachoanza mazoezi tayari kumenyana na Burkina Faso katika mechi muhimu ya kundi D kutafuta nafasi ya kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho kitaanza mazoezi yake katika uwanja wa Namboole siku ya Ijumaa jijini Kampala.

Mchuano huo utachezwa jijini Ouagadougou tarehe 26 kabla ya mchuano wa marudiano tarehe 29 katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.

Uganda inakwenda katika mchuano huu ikiwa inaongoza kundi hilo kwa alama 6, baada ya kushinda mechi zake mbili dhidi ya Bostwana na Comoros.

Kikosi Kamili:

Makipa: Dennis Onyango (Mamelodi Sun Downs, South Africa), Robert Odongkara (St George, Ethiopia) James Alitho (Vipers, Uganda), Salim Jamal (El Merriekh, Sudan);

Mabeki: Denis Iguma (Al Itihad, Lebanon), Isaac Isinde (St George, Ethiopia), Joseph Nsubuga (Bright Stars, Uganda), Joseph Ochaya (KCCA, Uganda), Denis Okot Oola (KCCA, Uganda), Isaac Muleme (SC Villa, Uganda), Murushid Jjuuko (Simba, Tanzania), Hassan Wasswa Mawanda (Al Shorta, Iraq), Timothy Awanyi (KCCA, Uganda), Bernard Muwanga (Bright Stars, Uganda);

Viungo wa Kati: Mike Azira (Colorado Rapids, US), Aucho Khalid (Gor Mahia, Kenya), Moses Oloya, Yassar Mugerwa (Orlando Pirates, South Africa), Tonny Mawejje (Knattspyrnufélagið Þróttur, Iceland), Ivan Ntege (KCCA, Uganda), William Luwagga Kizito (Feirense, Portugal), Mike Sserumaga (SC Villa, Uganda), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia), Farouk Miya (Standard Liege, Belgium);

Washambuliaji: Geofrey Massa (Bloemfontein Celtics, South Africa), Emmanuel Okwi (Sonderjsyke, Denmark), Erisa Ssekisambu (Vipers, Uganda), Hamis ‘Diego’ Kiiza (Simba, Tanzania), Ceasar Okhuti (KCCA, Uganda), Edrisa Lubega (Proline, Uganda).